MWONGOZO WA NOVELA”UTEUZI WA CHALE “-Asumpta K Matei.

MUKHTASARI.

Uteuzi ni neno linalotokana na neno teua yaani chagua.Chale ni mhusika katika novelahii.Uteuzi wa Chale ni uamuzi ambao mhusika chale alipaswa kuchukua katikakuchagua kipawa kipi angetumia ili kuitumikia jamii. Chale ambae ni mwanafunzi wa gredi ya saba anafahamika Kwa umaarufu wakekutokana na kipaji chake cha utangazaji.Yeye hutangaza au hupeperusha matangazo yamichezo ya vijana wanapokuwa wakijumuika pamoja katika michezo hiyo na kuifanyakufana zaidi na yenye mvuto.Wanapokuwa katika mashindano ya kuogelea katikabwawa la Mpingoni,yeye hupeperusha matangazo ya mashindano hayo ya kuogeleaakiwa kwenye jiwe maarufu lililofahamika kama ‘Sanduku la mtangazaji’.Aliyapambamashindano haya nakuyafanya yakuvutia zaidi hadi baadhi ya vijana wenzakewakambandika jina “mtangazaji mtarajiwa”. Siku moja Chale na wenzake wakiwa wametekwa na shughuli za mashindano yauogeleaji,walijisahau kuwa walifaa kuwatupia jicho ng’ombe na hivyo basi,ngombe haowakatokomea walikokwenda.Ghafla bin vu walilingundua hili na Ili kuepuka adhabuwatoto wenzake wakapiga lundi.Chale alimuona baba yake amefika bwawani lakinihakudhihirisha sura ya hasira.Mbali na hivyo Chale alivaa gwanda lake na kutoka shotimithili ya risasi.

Alfajiri iliyofuata Chale aliamka na maumivu makali ya mguu ambayo hata yeye mwenyewe alishindwa kung’amua chanzo chake.Baada ya babake Mzee Jibril na
mamake Bi Pili kuona maji yamezidi unga,waliamua kumpeleka mwanao katika kituo Cha afya Cha mwuguzi.Baada ya Daktari kumfanyia vipimo vya joto na vya mguu uliofura,akagundua kuwa joto lilikua juu sana na kuwa mguu ule haukuonyesha dalili yoyote ya kuteguka na hivyo basi akampatia mgonjwa dawa za kupunguza maumivu na kuwapatia barua ya kuwaamuru kuelekea hospitali kuu ya kaunti ili kufanyiwa uchunguzi wa kina.Daktari akawafahamisha kuwa huenda akahitajika kulazwa hospitalini huko Ili kurahisisha vipimo na matibabu jambo ambalo lilimshtua Chale. Katika hospitali kuu ya kaunti ya Heri wanakutana katika chumba Cha daktari na
daktari yuho huyo aliyemhudumia Chale katika kituo Cha afya Cha mwuguzi usiku uliotangulia.Si mwingine bali Daktari Maarifa.Chale alilazwa katika wadi ya st.Bakita Ili
kufanyiwa uchunguzi wa kina.katika wadi hiyo mwuguzi wake anakua ni sudi.Baada ya uchunguzi wa kina uliohusisha hadi baadhi ya vipimo kufanyiwa ng’ambo ,Daktari maarifa aliwabainishia wazi kuwa Mwanao Chale alikua na uvimbe kwenye sehemu inayounganisha wayo na muundi na kuwa uvimbe huo ulikuwa na seli za Kansa au
saratani na hivyo basi alihitaji upasuaji wa haraka. Siku ya oparesheni ilipowadia,Daktari Maarifa,na wenzake pamoja na sudi walijumuika katika chumba Cha oparesheni Kwa shughuli iliyotarajiwa.Daktari maarifa aliongoza
upasuaji huo ambao uliebuka kuwa wenye ufanisi na Daktari Maarifa akalitoa tufe lililokuwa limejificha kwenye sehemu inayounganisha wayo na muundi.Safari ya
kupona ya Chale ikaanzia hapo.Mzee Jibril na Bi Pili walijawa na furaha na ufanisi huo ijapokuwa Jibril alikuwa na hofu kuhusu malipo ya upasuaji kwamba yangekua
maradufu.Daktari Maarifa akawahakikishia kuwa gharama yote ya matibabu ilikuwa juu yake jambo lililowafanya kummimina shukrani sufufu. Baada ya Chale kupona na kutoka hospitalini,alirudi katika shule yake aliyokuwa
akisomea kabla ya kuugua.Walimu wakafikia uamuzi wa Chale kuendelea na gredi ya nane ijapokuwa alikuwa hajaisoma kikamilifu gredi ya saba.uamuzi huu uliafikiwa
baada ya wao kumhoji Chale na kugundua kuwa alikua akijiendeleza kimasomo alipokuwa hospitalini. Chale alikua na vita vikali kuhusu taaluma ambayo angependa kuiendeleza.Tokea alipopokea msaada mkubwa kutoka Kwa Daktari maarifa,alikua katika njia panda.Hakujua aendelee kupigania talanta yake ya utangazaji aliyoienzi au kujikita katika uwanja wa matibabu aweze kuokoa jamii.

Simu moja baada ya kupewa kazi ya utafiti shuleni kuhusu mangojwa ambukizi nakuibuka bingwa katika utafiti wake,azma yake ya kusomea taaluma ya matibabu ilikuaKwa Kasi mno. Chale alijiunga na Chuo kikuu Cha Seraji katika Kitiv o Cha Afya na Tiba.Huko Chuoni anakutana na mwuguzi na rafikiye sudi ambaye amejisajili kuendeleza taaluma yake yauuguzi.Chale alisomea taaluma ya upasuaji na matibabu ya viungo vya mwilivinavyohusiana na mkojo kama vile Figo,kibofu. Chale anamfanyia upasuaji daktari wake na rafikiye wa dhati Daktari maarifa aliyekuwana tatizo la uvimbe kwenye kibofu.Anafanikiwa na kuyaokoa maisha ya daktari maarifakama vile alivyookolewa maisha yake awali.Ama kweli wema hauozi.

UFAAFU WA ANWANI.

Je novela hii inaafiki anwani”uteuzi was Chale?” Ama kweli novela hii inasadifu anwani “uteuzi wa Chale” kwa kuwa
inamhusu mhusika Chale aliyekuwa na vipawa anuwai.Chale alihitajika kuchagua kipawa ambacho angeweza kukiendeleza katika kuihudumia jamii.Chale alikua na kipawa Cha Uogeleaji,Utangazaji,Utabibu na hata Ualimu Kwa kuwa alikuwa mfafanuzi mzuri wa mambo.Alihitajika kuchagua kipawa kati ya hivi
ambacho angeweza kukiendeleza Ili kuhudumia jamii.uteuzi huu ulimhusu yeye mwenyewe.Alipotaka ushauri kutoka Kwa babake,aliambiwa wazi ya kuwa vipawa vyote alivyo navyo ni muhimu ila katika uteuzi wa kipi angetumia ili kuihudumia jamii,ulikuwa mikononi make.Uteuzi ulikua wake,”Uteuzi wa Chale”.

DHAMIRA.

Dhamira ya mtunzi katika novela ya “Uteuzi wa Chale” ni kudhihirisha umuhimu wa kuvikuza vipawa kwa manufaa ya baadae na vilevile haja ya kukiteua kipawa mwafaka katika kuihudumia
jamii.